Aug 29, 2008

Saa ya ukombozi

Wakati umefika wa kujiuliza, kujitafiti, kujinasua na kujikomboa kutoka kwa hawa wanyonyaji makupe wanaotumia jasho letu kutunyonya ili wao waendelee kuwa matajiri, yatupasa kujiuliza kwa kina na fikra za kimaendeleo sasa tufanyeje? Kwani wa kutukomboa sasa hayupo tena kwani Azimio la Arusha mtetezi wa haki halipo tena!!! Wale makupe ngunguni wamelihujumu ili watunyonye kweli na sisi tunakubari Azimio la baba wetu Hayati Mwalimu JK Nyerere liondoke kwa sababu Mwalimu hayupo?

Tusikubari yatupasa kushika kila kitu kurudisha Mkombozi wetu Kipenzi Azimio la Arusha kwani alikuwa analinda maslahi yetuna jasho letu lisitumiwe na Wanyonyaji wa nguvu za umma, yatupasa kujiuliza ni lini tutajikomboa na kutoka katika Utumwa wa hawa Mabeberu wanyonyaji?

Sisi wenyewe ndio tunaweza kujikomboa kwa Azimio lilitufundisha Ujamaa na Kujitegemea kwahiyo tusisubili watu wengine watukomboe hayupo wa kutuhurumia tupambane ili tulirudisha Azimio la Arusha liunguze tena vikaragosi na kuleta ujamaa wa kweli. Ndugu wanaharakati, mashika ya dini, mashikaka mengine malimbali, na watanzania wote tupiganieni azimio la baba wa Taifa tuhakikishe tunalirudisha na kanuni zake za kukata milija kwa Mabwanyenye.

Tusiposimama imara kwa hili wataendelea kumdhalilisha baba wetu wa Taifa kwa kuvunja haki za utawala bora wenye kujali kila masilahi ya umma

Aug 27, 2008

Nguvu ya Fikra ni Ukombozi Daima



Watanzania wanadhulumiwa haki yao
Fita Lutonja


TANZANIA ni nchi yenye kila aina ya rasilimali. Ina madini, misitu, mbunga za wanyama, maziwa mbalimbali kama vile Victoria, Nyasa, Tanganyika n.k.

Vile vile ina Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kupita milima yote barani Afrika. Sifa nyingine ya nchi yangu Tanzania ni nchi ya amani kuzidi nchi nyingine ulimwengu kote. Ama kweli mimi ninajivunia kuwa Mtanzania.

Ndiyo maana namwomba Mungu aibariki Tanzania. Tanzania ina sifa nyigi sana tangu zamani enzi za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nyerere aliitakia mema Tanzania, alitaka Tanzania yenye neema, Tanzania yenye kukua kiuchumi, kisaikolojia, kiutamaduni, kijamii na kisiasa.

Lakini sasa hivi mbona mambo yamebadilika? Tanzania ya leo ipo tofauti sana na ile niliyoielezea hapo juu.

Sasa hivi Tanzania inazizima, inawayawaya, inavunjika sana, inatumbukia shimoni, inanuka kila aina ya mabaya; kuna ufisadi, kuna EPA, kuna mpasuko wa kisiasa Zanzibar, kuna Richmond, kuna suala la Zanzibar ni nchi au si nchi, kuna suala la vijisenti vimefichwa Uingereza, kuna suala la Mkapa na mke wake kufanya biashara Ikulu ya Tanzania, na mengine mengi. Yote haya mbona Tanzania mnatuchanganya?

Au mumeamua kufanya hivyo kwa sababu Baba wa Taifa hayupo? Au kwa sababu mlivunja Azimio la Arusha ambalo lilikuwa linabana na kudhibiti ufisadi?

Mwalimu aliona mbali sana. Mlipovunja Azimio la Arusha ninawauliza mlitaka kila mtu ajichukulie chake? Kwa sababu ya nani haya yanatokea sasa? Tumlaumu nani kwa haya yote? Sasa mnatupeleka wapi, mbona sisi wananchi wa kawaida hatuwaelewi, mnaendelea kutuumiza!

Sasa Watanzania wanalikumbuka Azimio la Arusha. Mwalimu aliona mbali sana kipindi cha utawala wake ndiyo maana alianzisha Azimio la Arusha.

Aliona kuwa kunaweza kutokea watu wasiojali masilahi ya Watanzania wengine; walafi, mabepari, mabwenyenye, wenye fikra mbaya kwa wengine, wenye kutafuna taifa kwa kutumia dhamana ya uongozi na kusababisha Tanzania kuyumbayumba.

Watanzania sasa wanamkumbuka Baba wa Taifa kwani wanaamini angekuwepo asingevumilia mambo kama haya ya ufisadi, ambayo alikuwa anayapiga vita sana kwa nguvu zake zote.

Ninakumbuka Mwalimu baada ya kuona mambo kama haya ya ufisadi, unyonyaji n.k. yatatokea, bila ajizi aliitisha mkutano Arusha na kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967.

Lilipotangazwa, wananchi wanyonge wa nchi hii, walirukaruka na kushangilia. Wananchi hao walishangilia kwa sababu waliposikia misingi ya Azimio hilo, walifahamu fika kuwa ndio ukombozi wao.

Walikuwa bado wana machungu kutokana na kunyonywa, kundamizwa, kunyanyaswa na kudhulumiwa ndani ya nchi yao wenyewe.

Walikuwa bado wana kumbukumbu za ubeberu na ukoloni ambao ulikuwa umeota mizizi na pamoja na kuwa nchi ilikuwa huru, lakini watu wengi walikuwa bado hawajaanza kufaidi matunda ya uhuru, hasa katika nyanja ya uchumi, kwa sababu yalikuwa bado mikononi mwa watu wachache.

Watanzania wanakumbuka Azimio lilisababisha kuzaliwa kwa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii iliwawezesha Watanzania kushirikiana kwa kila jambo na hivyo kujenga udugu uliowafanya Watanzania wajione kuwa kama watu wa familia moja. Vilevile kujitegemea kulisababisha Watanzania kuishi kwa kujiona wao ni wao. Dhamira yao kubwa ilikuwa ni kujenga uwezo wao, ili waachane na utegemezi wa nchi nyingine. Walifahamu kuwa huo ndio uhuru wa kweli.

Ili kuhakikisha kuwa linaondoa kabisa chembe chembe za unyonyaji, Azimio la Arusha liliweka kanuni zilizokuja kujulikana kama maadili ya uongozi kwa watumishi wa umma. Kanuni hizi zilitaja mambo ambayo mtumishi wa umma, hasa kiongozi, haruhusiwi kuyafanya.

Hii ililenga kuhakikisha kuwa viongozi hawatumii nafasi walizonazo kujigeuza mabeberu, wakiritimba na wanyonyaji. Jamii iliwahakikishia viongozi kutunzwa kupitia mishahara yao. Pia dhana ya Ujamaa na Kujitegemea iliwahakikishia viongozi kuwa watakuwa sawa na wananchi wengine wanawaongoza. Azimio la Arusha lilizuia kujengeka kwa matabaka katika jamii ya walionacho na wasio nacho.

Lakini hivi sasa nchi inayumbishwa na ufisadi, unyonyaji, ukandamizaji. Watu wameshaanza kumkumbuka Baba wa Taifa. Tunajiuliza tumekosea wapi? Inaleta hisia mbaya zaidi pale ambapo wanaoonekana kuwa vinara wa ufisadi na unyonyaji ni viongozi ambao tuliwakabidhi dhamana ya kutuongoza.

Mwalimu ndani ya Azimio la Arusha na kanuni zake aliamini kuwa Watanzania wataishi kijamaa kwa kushirikiana kwa kila kitu. Alilenga kujenga umoja chini ya upendo wa kidugu. Katika mazingira kama hayo, kwenye dhamira ya dhati kabisa, isingekuwa rahisi kwa viongozi kuwageuka watu wao na kuanza kuwa wajasiriamali zaidi ya viongozi.

Azimio la Arusha la Baba wa Taifa lilikataa ubaguzi wa mtu na mtu. Lilipinga unyonyaji wa mtu na mtu. Kitu hiki kilisababisha Watanzania kipindi hicho kuwa na amani katika maisha yao, huku wakiishi kwa kupinga aina zote za dhuluma.

Lakini hivi sasa, amani hiyo ipo mashakani. Wananchi wa kawaida waliotopea katika umaskini wanapowaona viongozi wao wakiogelea katika ukwasi wa hali ya juu, huku wakihubiri umaskini, wanachanganyikiwa. Lakini viongozi wanapaswa kushikwa na hofu kwamba amani imeshaanza kutoweka.

Unapoona watu wanamwadhibu kibaka aliyeiba kuku mtaani kiasi cha kufikia kumuua kwa kumchoma moto, ujue siku itafika ambapo watafanya hivyo kwa wezi wakubwa wakubwa na wala rushwa wakubwa wakubwa. Kwani lengo lao si ni kutoa adhabu kwa wahalifu?

Viongozi wanatakiwa waanze kukaa chonjo hivi sasa. Vita dhidi ya ufisadi iliyoanza, haitakoma mpaka wananchi wa takaporidhika kuwa ushindi umepatikana kiasi cha kutosha.

Salama ya viongozi ni kujiuliza nani alivunja hili Azimio la Arusha? Wanatakiwa kueleza kinagaubaga kwa nini Azimio lilivunjwa? Huyo aliyelivunja alikuwa anawatakia nini Watanzania?

Aliyevunja azimio letu jema atuambie alikuwa ana makusudi gani kufanya hivyo? Hivi alikuwa anatutakia ufisadi, ubepari, ubeberu na mambo ya EPA? Au alitaka kuona Tanzania inawayawaya na kufikia hatua ya viongozi kuanza kufanya biashara Ikulu?

Ndiyo. Haya yote yanatokea hivi sasa kwa sababu ya kuvunjwa kwa Azimio la Arusha kwani Azimio lilikuwa halitaki mambo haya yote.

Hakika Mwalimu alikuwa anaipenda Tanzania, mbona hamkumuenzi Mwalimu?

Mnataka kutuambia kumuenzi Mwalimu ni kufanya biashara lkulu na kumiliki migodi? Mbona Azimio la Arusha lilikuwa halitaki hivyo?

Baada ya Mwalimu kung’atuka madarakani, tumeona yale ambayo alikuwa anayapiga vita yakianza kujitokeza taratibu na alipofariki yakashika kasi. Kasi ya mambo aliyoyachukia Mwalimu iliongezeka zaidi pale walipoamua kulivunja Azimio la Arusha. Wakati azimio hili lilitangazwa kwa mbwembwe zote mwaka 1967 wakati linazaliwa, lilipofutwa hata haikutangazwa!

Walikutana kimya kimya wakasema Azimio linasababisha watumishi wa serikali wakose nyumba pindi wanapostaafu. Sasa tunagundua kuwa walikuwa na nia ya kuweka misingi ya kuiba mali ya umma wakati wakiwa kazini!

Hao watu eti nao wanajiita wazalendo? Kutuvunjia misingi ya utawala bora ili muibe na kuwa mabepari, ndio uzalendo? Kuficha pesa katika benki za nje ndio uzalendo? Kujenga majumba makubwa kama mahekalu na kusomesha watoto wenu nchi za nje kwa pesa za walipa kodi ndio uzalendo? Tuelezeni Watanzania, huo ndio uzalendo wenye itikadi ya kufia nchi yako kwa kuitetea?

Kwa mimi ninavyoamini uzalendo ni ile hali ya kuwa tayari kuifia nchi yako. Kwani katika Tanzania hii hamuoni wazalendo? Hamuwaoni kina Dk. Willibrod Slaa kuwa hao ndio wazalendo?

Hamuoni kuwa wako mbele kutetea maslahi ya nchi yao? Hamuoni Baba wa Taifa kwa kuanzisha Azimio la Arusha kuwa alikuwa mzalendo? Hamuoni Edward Sokoine na kazi aliyoifanya kuwa ni mzalendo?

Kwakweli mmetufikisha pabaya sana na tunasema hatutaki kuendelea kusikia mambo ya ubepari, unyonyaji, ufisadi, EPA, biashara za Ikulu, mpasuko wa kisiasa Zanzibar na matatizo chungu nzima.

Makala hii imeandaliwa na mwananchi mwenye fikra za maendeleo. Anapatikana kwa simu: 0764 992264

Aug 23, 2008

Muda ni mali

Muda ni mali na heshima kwa watumia vizuri muda wao, hakika ukitumia muda wako vizuri utapata mafanikio na ukikata tamaa na kuaanza kulalamika hakika utabaki hivyohivyo tu yatupasa kuutumia muda wetu vizuri na hasa katika suala kujinasua katika umaskini sijalishi umaskini wa mtu mmoja pekee, hakuna bali ni umaskini wa Tanzania.

Tuijenge nchi yetu kwa kujituma kila sehemu kuhakikisha kunaijenga hata katika nyanja za kuhakikisha wanyonyaji tunawafutilia mbali, unyonyaji huu wa mabeberu yatupasa kuupinga kwa nguvu zote kwani hawa ndio chanzo cha umasikini wetu.

Sisi wazalendo tunabaki maskini huku wao wanatunyonya kila kona huku wakitutumikisha kwa malipo duni, sasa yatupasa kujikomboa kwa kudai Azimio la Arusha la baba wetu wa Taifa hayati Mwalimu J.K. Nyerere kwani hili lilikuwa mzingiti wa kukomesha unyonyaji wa mapepari na waliovunja hili Azimio yatupasa na wenyewe kuwazomea hadharani ili waone aibu ya kuvunja utawala bora wa kijamaa huku wakitupigilia kichwani mwetu bila huruma, misumari ya wapepari sijui walikuwa na ajenda gani na hawa mapepari au na wao ni mabepari?

Wajibu wa kijana

Kwanini kijana unakaa vichochoroni, unalala mitaroni, unabeba zege na magunia, unasukuma matololi, unakimbizwa na migambo wa mji, unatembea kwa miguu bila kupanda daladala, unashinda kutwa nzima hujatia kitu tumboni huku tumbo linakuuma na huku nguvu zinakuishia taratibu unaelekea guanguka??? Yote haya ni mfumo mbaya ndio unaokutesa kijana wangu na sioni pa kijikomboa!!!!!!

Kijana wangu inaniuma sana ninapokuona unanyanyaswa na hawa fisikoko hawayani, wezi wakubwa wa raslimali zetu ambazo Mungu alitupatia wao wanazitumia bila kukuhurumia wewe kijana na wanataka wakumalize kwa njaa ili wajitwalie raslimali zetu bila kipingamizi, sasa tuwazomee haoooooooooo weziiiiiiii wakubwaaaaa tumewashutukiaaaa sasa hatutaki kuibiwa kwani hawa ni wabaya sana wanatudanganya kwa mikataba mibovu huku wakiendelea kutufirisi mali yetu, ukienda Buzwagi wanaiba, Bulwanhgulu wapo, Geita wanaendelea kusafirisha dhahabu zetu, Mlima Ngasamo na Mererani wamejaa huku sisi tunakufa na umaskini.


Sasa kijana simama imara uitetee haki yako, wote vijanawa kike na wakiume pambaneni na mafisadi na wizi wa madini yenu hapo ndio hadhi yenu itarudi na mtakula haki yenu, ninasema we kijana acha kusinzia, acha kudhurura, acha kukaa, acha kujiona huwezi kutetea haki yako daima pambana kwa nguvu zote kurudisha heshima na uhai wako hakika utajikomboa.

Aug 22, 2008

Tanzania Wanakutolea macho

Tanzania mbona wanakutamani kila sehemu ya dunia? Mabeberu na Mabepari wametoa macho juu yako, huku wakija kwa nguvu wakitaka kukudhulumu haki yako wengine wanajifanya kuwa rafiki zako ili wakudhulumu raslimali zako ulizonazo, wanakudanganya kwa kukupa zawadi ndogo ili kukupumbaza, wakuibie.

Ninajiuliza ni kitu gani ulichonacho mpaka wanakutamani na kutaka kukuibia? Aaah kumbe ni raslimali zako ndizo wanazitamani!! basi unasitahili pole na kuhurumiwa sana Tanzania.

Angalia sasa ulipowakubali na kuwapokea kwa mikono miwili wameanza kukudhulumu mali yako na kupeleka ughaibuni huku wakikuacha wewe umejikaukia ka!! bila hata huruma. Kukauka kwako kumekufanya uwaombe misada hao wezi wa mali yako, napo unapowaambia wanaaza kukucheka na kukusema Ehee!! Eti wewe ni maskini omba omba wakati wao ndio wamekukausha na kukufirisi raslimali zako, lakini usijali Tanzania wangu nikupendae kwani hohehahe hakoswi siku yake, ipo siku tutachoka kunyonywa na kudhulumiwa haki zetu hapo ndipo tutapambana nao usiku na mchana ili kukukomboa wewe Tanzania.

Tanzania ya dhamani

Tanzania wewe ni wa dhamani sana hakika Mwenyezi Mungu alikujaria na kukubaliki tena kwa upendeleo, kwani kila kitu alikupatia, madini ya kila aina alikupa, mito na maziwa ya maji na zenyewe alikubariki, mbuga za wanyama kubwa zenye kuvutia kila aina ya watarii, ardhi yenye rutuba sanjari na milima mbalimbali ukiwemo mlima mrefu kupita yote Africa Kilimanjaro alikupa hakika wewe Tanzania umebarikiwa.

Lakini mimi ninakushangaa Tanzania pamoja na vitu vyote hivyo bado unaendelea kuisha na kubakia mashimo kila sehemu, huku madini wakikunyang`anya na kupeleka ughaibuni kama wewe huna watu wako!!?? hakika ninakusikitikia Tanzania wangu kwa jinsi unavyokaukia na kukonda huku ukibaki mifupa tupu!!!! samaki wako sangara wanakwapuliwa, pesa za walipa kodi wako zinafisadiwa na mafisadi wahujumu mali zako, ooooo!!!!! Ona sasa umebaki maskini huku ukiwayawaya huna pa kukimbilia!!

Ninazidi kushangaa sana wale waliokunyonya wanatembelea benzi, crusser,prado vx zenye mabillioni ya pesa zako ukiwasachi kwenye mabegi yao wanayotembea nayo yamejaa pesa zako huku wakiendelea tena kukutwisha mzigo kichwani wa makapuni yanayokufirisi, huku wewe ikibaki umekonda huna hata kitu cha kuwapa Watanzania!! Sasa yakupasa upambane na wanaokufirisi kwani watu wako watakufa kwa njaa. Haya jamani Watanzania simameni kuikomboa Tanzania Dr. Wilbroad Slaa simama, Zitto Kabwe inuka, Anne Kalango, Harisoni Mwakyembe, na wanaharati wenzanu simameni kupambana, Tanzania inaisha huku tunaiona mafisikoko wanaitafuna bila huruma kabisa.

Aug 21, 2008

Lenin na Marx

Huwa ninalia ninapowakumbuka wapigania haki za wanyonge kama Lenin, Fredrick Angle, Dk.Carl Marx, Josef Stalen na wengine wegi huwa ninawakumbuka sana japo sitakufahamisha ni kitu gani walikifanya katika kupigania haki za binadamu kutoka kwa Mabepari ninajua bila shaka unawajua umuhimu wao katika jamii.

Lenin aliweza kupambana na mabrpari wa Urusi kwa mantiki ya kuondoa unyonyaji katika harakati zake aliwahi kuwekwa zizuizini, kufukuzwa chuo alikokuwa anasomea shahada ya sheria na kudhalilisha sana, naye Dk.Carl Marx alikuwa kama Lenin mpaka aliwahi kuandika kitabu cha kilichokuwa kinapinga unyonyaji wa Mabepari. Daima huwa ninafarijika sana ninapokumbua watu hawa muhimu katika historia ya haki za binadamu na huwa ninapata nguvu na msukumu wa kwamba kumbe hata sisi tunaweza kukomesha unyonyaji.

Habari njema

Habari zenu ndugu zangu popote pale mulipo mimi ni mzima na ninaendelea na pilikapilika za kuhakikisha haki inapatikana kutoka kwa wanyonyaji wetu wanajiita Miungu watu na kijiona wao ndio Mungu amewajalia na kuwaona na kutuona sisi kama Mungu hatupendi kumbe wanajidanganya wao wenyewe kwani Mungu wetu aliyembinguni anatupenda wote ndio maana akatupa kila kitu wote lakini wao kwa kumuuzi wakaamua kutunyang`anya na sisi haki yetu.

Watu hawa sasa wanafurahia katika dunia hii hawajui kuwa dunia hii ni ya kupita tu na makao yetu ya kudumu yako mbinguni kwa baba yetu Mungu, kule mbinguni ndio kutakuwa hakuna tena unyonyaji kama wanavyotufanyia sasa hivi huku wakitoa meno yote 36 nje kwa kujiona wao ndio wajaja kuzidi wote katika dunia hii.

Chama ni moyo

Ili kujikomboa na wanyonyaji yatupasa kuwa na umoja wenye mshikamano wa dhati umoja huo unakuja kwa kuunda chama kwahiyo wanaharakati wenzangu yatupasa sasa kuunda chama chetu cha kudai masilahi yetu wanayoyatumia kama sisi hatupo katika dunia hii kwani kimya chetu kimewafanya watuone hatuna haki.

Lakini katika maono yangu ninaona haki a wanyonge inakuja kwa nguvu zote ninaona uhuru wa kutoa maoni umekalibia watu watajikomboa kutoka kwa mabeberu makiritimba, manyonyaji, mabepari na wapinga haki yetu tuliyopewa na Hayati Mwalimu JK nyerere baba wetu wa Taifa mwenye kila aina ya sifa za kuitwa kiongozi bora Afrika. Je ninawauliza hao wabepari na wabeberu wa nchi hii huu ndio usawa wa binadamu? Mbona wenzetu mnadhurumu huku tunawaona?

uhuru na haki: Machozi yetu yasamani

uhuru na haki: Machozi yetu yasamani

uhuru na haki: Machozi yetu yasamani

uhuru na haki: Machozi yetu yasamani

Aug 20, 2008

Dhambi ya ubaguzi

Rasilimali zetu wao wanaona kama Mungu aliwapa wenyewe na sio Watanzania wote. Wanajiamulia katika rasilimali zetu bila hata sisi kuwaruhusu wenyewe wanachukua huku wakituona sisi kama hatuna haki nazo, wakati Mungu alipotupaeia alitupa sote watanzania bila kubagua. Sasa wanaleta utawala wa kibaguzi kwa kutubagua wajili wao wakuu wakiwa na fikra za kuwa sisi ni wajinga hatujui haki zetu kumbe tunajua kila kitu, haya sasa Mungu ameshawalaani kwa kosa la kutubagua katika mali zetu, utawala wo umejaa fitna na unanuka ubaguzi kila sehemu.

Waonini sasa wamemukufuru hata Mwasisi wetu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Watanzania kwa kushindwa kumuenzi kwa kila kitu, nakumbuka Mwalimu katika utawala wake alikuwa anapinga sana utawala wa kibaguzi, alimchukia kila mtu atakayeonekana mubaguzi kwani aliamini binadamu wote ni sawa,nakumbuka aliwahi kusema kuwa dhambi ya ubaguzi ni kubwa mno kwani ni sawa na mtu kula nyama ya mtu ambaye akiisha ila hataiacha katu.Hii ni kweli kabisa viongozi wetu mumezoea ubaguzi munatubagua sisi na hamtaacha kutubaguaa mpaka tujikomboe hapo ndio haki yetu itatimia

Hakika tunaweza

Ninaimani kubwa sana Watanzania tunaweza kujikomboa na kuwa huru kifikra, kimawzo, kiuchumi, kisansi, kijamii, kisaikoloa nk, ili tujikomboe yatupasa kufikria ni viongozi gani wanatufaa? ambao watasimama kutetea haki zetu na rasilimali zetu? hakika tukijua hilo hapo ndipo tutajikomboa na kuwa huru katika haki zetu, lakini tusipojua hilo daima tutaendelea kudhulumiwa haki zetu kwani viongozi wetu hawana na huruma nasisi pamoja na watoto wetu.

Lakini hawa wanyonyaji ninawaambia siku zao zinahesabika hazikawii ukombozi wetu unakuja mbio sana kwani hata wao wenyewe wanajua sehemu walivyotukosea sasa wanawayawaya hawana imani na sisi wameanza kutuhofia kuwa hueda tukafanya mapinduzi ya kura mwaka wa uchaguzi unaofuata.

Tumechoka kudhulumiwa

Tanzania ina kila kitu Mungu kaijalia kuwa na kila kitu ina mito na maziwa wa maji nyenye kila aina ya samaki, madini ya kila aina almasi, tanzanite, dhahabu, ulanga, makaa ya mawe,shaba, rubi nk vilevile ina milima mingi kama vile mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kupita milima yote Afrika, mbuga za wanyma nk, vyote hivi ni mali za watanzania lakini ninashindwa kujua umasikini wetu umetoka wapi? Nani mchawi wa umasikini wetu? kwangu mimi ninavyoona mchawi anayesababisha umasini ni wale viongozi wetu hawafuati misingi ya utawala bora wenye kulinda mali hya umma bali wanauza mali zetu na kusingizia uwekezaji. uwekezaji huku munaliingizia Taifa hasara kwa mikataba mibovu lakini tunawatahadhalisha ole wenu nyinyi wanafiki ipo siku Mungu atawaadhibu kwa niaba ya watanzania, hapo ndio mtakoma na kujuta kwanini mlizaliwa Tz, lakini sasa munachekelea huku mukiendesha magari yenu ya kifisadi na kutaka kutugonga huku mukitutukana iti sie washezi, washamba hatujui hata kukwepa magari.

Aug 19, 2008

Machozi yetu yasamani

Ni nani asiyelia anapo pigwa na kuumizwa? kwanini tusilie munapotupiga kwa kutudhurumu mali zetu. Yote haya ni maisha ya nini tuchekane? Tunahuzunika sana Tunapoona wenzetu mnatucheka hata pale tunapowaona wanyonyaji munatucheka huwa tunapata hasira kubwa sana kwani nyinyi nii wadhulumaji wetu, kwanini munatucheka tena? Sasa ninasema kuchekwa nimechoka ninahitaji kujikomboa.

Aug 12, 2008

Uhuru na haki

Uhuru na haki ni vitu ambavyo zinaendana sisi binadamu yatupasa kuzingatia mambo kama haya, uhuru ni njia pekee inayoleta ukombozi, binadamu anajikomboa pale anapojua kuwa hayuko huru, hapo ndio hupigania haki yake ya kuwa huru,kwahiyo binadamu wote dunia nzima yatupasa kutambua kama tuko huru kifira, kiuchumi, kisiasa, kisaikolojia, nk pale unapotambua kuwa hauko huru basi yakupasa kusimama na kupigania uhuru wako jua kwamba unapo kuwa huru na haki inakuwepo