Sep 11, 2008

Ukombozi wa haki ni uhuru wa habari

MAKALA

KWA misaada mbalimbali ya habari tunaona historia ya mawasiliano ya umma ilianza mwanzoni mwa utamaduni wa watu walipokuwa wanawasiliana na mfumo wa ishara baadaye wakawa wanawasilia kwa mdomo kipindi hicho kulikuwa hakuna lugha ya kuandika , kwahiyo mawasilia yalifanyika pale watu wanapoonana oso kwa uso

Kipindi hicho watu walikuwa wanaishi kwa kutegemeana lakini kulingana na muingiliano wa jamii mawasiliano yalihitajika sana mwingoni mwa jamiiambapo mawasiliano hayo kulingana watu kuhitaji kuwasiliana, mawasilano hayo hayo yalihitaji teknolojia zaidi ili kukidhi mahitaji ya jamii.

Miongoni mwa miaka ya 5,000 kabula ya Christo sehemu mbalimbali binadamu waligundua herufi mbalimbali kama kule Misri watu wa kule waligundua herufi za kutumia picha ambazo walikuwa wanatumia katika kufikishana ujumbe. Huko China watu wa kule waligundua herufi mbalimbali ambazo walitumia katika mawasiliano yao, hii yote inatudhihilishia kuwa watu walihitaji sana kuwasiliana na inatuonyesha kuwa mawasiliano ni ya muhimu katika jamii hayapaswi kupuuzwa hata kidogo kama yanavyopuuzwa Tanzania.

Halikadhalika siku zilivyozidi kwenda ndio watu walivyokuwa wanahitaji zaidi mawasiliano miongonui mwao hapo ikaja pale Mwanamapinduzi Mhunzi wa vyuma Johannes Guernberg alipokundua mashine ya kuchapisha herufi ambayo ilisaidia sana watu katika kuwasilia kwa kuandika hizi ni changamoto zilizojitokeza ili kuhakikisha binadamu anapata mawasiliano.

Ugunduzi wa Guternberg ilivuta hisia kubwa sana miongoni mwa jamii ambapo watu wengi walikubali ugunduzi wake. Mitandao mbalimbali inatuambia miongoni mwa watu waliokubali kazi ya Guternberg ni Mwanaharakati Marshall McLuhan ambaye alielezea kuhusiana na kazi ya Guternberg katika kitabu alichokiandika mnamo 1962 huku akikiita kw jina la “The Guternberg Galaxy” katika kitabu hiki McLuhan alielezea kiundani zaidi umuhimu wa ugunduzi wa Guternberg katika mfumo mzima wa mawasiliano.

Mitandao inaendelea kutuhabarisha kuwa uvumbuzi wa Guterberg ulipelekea kujitokeza kwa uandishi wa habari ambapo ilipelekea kuanzishwa kwa machapishi mbalimbali, kuko Kaisari Roma kulianzishwa gazeti la Acta Diurna na sehemu mbalimbail kama huko Holland mwaka 1920 kulianzishwa gazeti la Corantos. Hii yote ilikuwa ni kupanuka kwa mawasiliano kutokana na mahitaji ya binadamu, ambapo ilipelekea baada ya muda kujitokeza kwa uandishi wa habari na vyuo mbalimbali za uandishi wa habali zikaanzishwa, ilikuweka mbele umuhimu wa mawasiliano na kuwawezeshha waandishi kuwa makini na kazi yao.

Kulingana na kupanuka kwa mawasilano ya habari kwa kutumia vyombo vya habari na vyuo vya uandishi wa habari kuongezeka Taaluma hii ya habari ilipata umuhimu zaidi na kuleta changamoto kubwa sana miongoni mwa jamii. Huko marekani taaluma ya habari ilitiliwa maanani sana, siyo tu Marekani hata nchi zingine ziliona umuhimu wa taaluma hii yenye kutumia hakili na busara, kuwa ni miongoni mwa taaluma ya muhimu sana katika jamii. Baada ya kuelezea hayo hapo juu kama nilivyokufahamisha hapo mwazo kwamba nimetumia vyanzo vya habari mbalimbali ikiwemo mitandao.

Ninakuja sasa Tanzania. Je, hii taaluma tunaidhamini kama nchi zingine? Tunaipa heshima kama taaluma zingine kama vile udaktari, ualimu, uchumi, uongozi, Uanasiasa, utaalamu wa miamba, uiginia, nk? Tanzania hii taaluma ya habari haidhaminiwi, inatukanwa, inadharauliwa, inanyongwa hadharani, kudharauliwa hivyo ndio inapelekea taaluma hii kuonekana dampo kwa kila Mtanzania, ninaposema dampo musinielewe vibaya mbali ninamaana ya kuvamiwa na kila mtu na kujiita Mwandishi wa habari. Ninarudia tena kusema kuwa taaluma hii Tanzania ni dampo, kweli hii taaluma ni dampo kabisa, tena lile dampo lenye kila aina ya takataka mbalimbali zikiwemo zile zinazonuka vibaya sana.

Hii inashangaza sana kwa nchi kama Tanzania kutothamini taauma ya habari ambayo ni taaluma muhimu sana ndani ya jamii kwani taaluma hii ndio mfanisi mkuu wa kuhabarisha Taifa katika nyanja mbalimbali kama vile za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kisaikulojia, kijeshi nk. Inashangaza sana kwa taaluma hii nyeti hapa Tanzania kuingiliwa na kila mtu kuanzia mtu wa darasa la saba utakuta ni Mwandishi wa habari na tena kaajiliwa na chombo cha habari. Huyu mtu darasa la saba hana taaluma ya habari atawezaje kuandika habari zenye kuelimisha jamii kama siyo kuidhalilisha taaluma ya habari na kuliweka Taifa katika hari ngumu? Huyu mtu darasa la saba hana upeo na suala zima la habari atawezaje hata kumuuliza maswali Waziri au Mkurugenzi yoyote ili apate habari yenye kuelimisha jamii? Ataanzia wapi kuuliza maswali wakati hajui namna ya kuuliza maswali yenye kupelekea kuandika habari yakinifu yenye faida kwa wananchi na Taifa kwa ujumla? Tunapofanya hivi siku za mbele Taifa litakuwa katika hari gani? Je litaelimishwa au litahatarishwa?

Tanzania kuna mambo ya ajabu kabisa utakuta hata mtu amesoma taaluma nyingine lakini mtu huyo akikoswa kazi katika fani yake anakimbilia uandishi wa habari, huyu atafanyaje kazi ya uandishi wa habari wakati fani yake ni Ualimu au Uasikari kama siyo kupeleka Taifa shimoni na kudidimiza uhuru wa wananchi katika kupata habari za kuelimisha ambazo ni haki yao ya msingi? Wanapokosea hawa watu ambao hawana taaluma hii ya habari si Taifa na Watanzania wote wanadanganywa? Tanzani tusifanye mchezo kwa mambao muhimu katika Taifa kama haya. Kwa nchi kama tanzania si ajabu kukuta chombo kama redio hakina Mwanataaluma wa fani hiyo hata mmoja, hivi vyombo vipo tena vingi!!!!! na vimesajiliwa na serikali yetu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Serikali inasajiri vipi hivi vyombo vya habari bila hata mwandishi na mtangazaji wa habari hizo kama siyo ufisadi ndani ya serikali na vyombo vya habari kwa ujumla? Hii si kufanya taaluma hii kama dampo la kukimbilia watu wa aina mbalimbali na matokeo yake kupata habari za uongo zenye madhara katika jamii. Serikali ninawaomba muangalie vizuri taaluma hii ya habari kwani musipoangalia mutajikuta munawaandihi wegine kutoka Milembe Dodoma!!!!! Maana uandishi wa habari umezidi kuvaniwa na kila mtu.

Tanzania hii taaluma imekuwa kimbilio la kila mtu (dampo) kwani hata mtu alikuwa anagombania ukisura (usura) akishinda huo usura basi anakuwa mwandishi wa habari na anaajiliwa na chombo cha habari. Hivi kushinda huo usura ndio kamaliza chuo cha uandishi na utangazaji wa habari? Mbona watu hawa wanadhalilisha taaluma ya habari? mbona hawakibilii uhakimu, ualimu au upolisi? Taaluma hii ya habari tunaididimiza wenyewe kwa kutoipa chamgamoto za kutosha na kuidhamini kama taaluma zingime, hii ndio inapelekea kudharauliwa kwa Waandishi wa habari wetu na kudharauliwa huko kunawalenga wanahabari wote kumbe wachafuzi wa taaluma ni wengine ambao hawajasomea taaluma ya habari na hawafuati maadili ya uandishi wa habari.

Kulingana na taaluma hii kuonekana ni taaluma ambayo inavamiwa na kila mtu serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari nchini waweke mikakati ya kudhibiti kuwa na waandishi wasio na taaluma ya habari katika vyombo mbalimbali vya habari hapo ndio tutalinda heshima ya kazi ya uandishi wa habari na wananchi tutawapa haki yao ya kupata habari zinazotakiwa lakini sasa Wananchi tunawnyima haki yao ya kupata habari zenye kuelimisha zilizoandikwa na kutangazwa na waandishi wenye ujuzi na taaluma yao. Tukifanya hivi hakika laana tutazimaliza zak kila siku kutukanwa kwa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya habari, utamatuni na michezo mwaka 2008/2009 iliyowasirisha bugeni inaonyesha dhahiri katika vyombo vya habari kuwa watatekeleza mambo mengi sana likiwemo la kulinda maadili ya uandshi wahabari hili linatakiwa liende sanjari na kuondoa waandishi wachafuzi wa maadili ya uandishi wa habari ili kuwatendea haki yao wananchi ya kupata habari zenye kukidhi mahitaji yao. Musituambie kuwa kazi ya uandishi wa habari inaweza kufanywa na kila mtu, hilo hatukubaliani nanyi hata siku moja, anayesema hivyo daima tutamuona haitakii mema Tanzania au hajui undani wa kazi hii, ama hajasoma uandishi wa habari ndiyo maana inataka kuingiza nchi katika janga ambalo watoto wetu watakuja kulijutia na kulaani kwa nini tulifanya hivyo? daima hii laana tutatembea nayo.

Pamoja na bajeti hii kuwa nzuri ili waandishi wa Tanzania waweze kuheshimika miongoni mwa jamii, serikali kwa kupitia wizara husika inatakiwa kuweka mipaka katika vyombo vya habari kuajili watu wenye taaluma ya habari na kuondoa fikra za kuamini kuwa kazi ya uandishi inaweza kufanya na kila mtu kwani tunapoamini hivyo tunakuwa hatuwatendei haki yao wananchi ambayo wanatakiwa kuipata kupitia vyombo vya habari.. Serikali iwajari wananchi wake kwa kuweka mikakati ya kuwapatia habari zenye mantiki ya kuelimisha, kuwafahamisha, kuwajenga kwa kuweka mikakati dhabiti kwa kuajiri watu wenye taaluma ya habari, kwani hao watu watakuwa wanaujuzi na kazi yao, wanajiamini na kuheshimu taaluma yao, hapa ndipo wananchi watapata habari zenye kuaminika na hii itapelekea kujenga heshima kwa waandishi wa habari .

Bila hivyo waandishi wa habari wataendelea kutukanwa, kunyimwa haki yao, kulaaniwa, kuwekwa kitanzini, kufukuzwa ofisini, kunyimwa uhuru, kudhalilishwa, pamija na kuitwa majina mengi ya kejeli na dhihaka kama vile makanjanja, wachovu, watu wa mishiko, waandishi njaa, chakupewa na mengine mengi wanayoitwa sasa hivi. Kejeli hizi zinawanyima haki yao waandishi wenye taaluma ya habari vilevile zinavunja misingi ya utawala bora Tanzania.

Toa maoni yako kwa kubonyeza sehemu ya maoni chini au nipigie 0764 992264