Aug 22, 2008

Tanzania Wanakutolea macho

Tanzania mbona wanakutamani kila sehemu ya dunia? Mabeberu na Mabepari wametoa macho juu yako, huku wakija kwa nguvu wakitaka kukudhulumu haki yako wengine wanajifanya kuwa rafiki zako ili wakudhulumu raslimali zako ulizonazo, wanakudanganya kwa kukupa zawadi ndogo ili kukupumbaza, wakuibie.

Ninajiuliza ni kitu gani ulichonacho mpaka wanakutamani na kutaka kukuibia? Aaah kumbe ni raslimali zako ndizo wanazitamani!! basi unasitahili pole na kuhurumiwa sana Tanzania.

Angalia sasa ulipowakubali na kuwapokea kwa mikono miwili wameanza kukudhulumu mali yako na kupeleka ughaibuni huku wakikuacha wewe umejikaukia ka!! bila hata huruma. Kukauka kwako kumekufanya uwaombe misada hao wezi wa mali yako, napo unapowaambia wanaaza kukucheka na kukusema Ehee!! Eti wewe ni maskini omba omba wakati wao ndio wamekukausha na kukufirisi raslimali zako, lakini usijali Tanzania wangu nikupendae kwani hohehahe hakoswi siku yake, ipo siku tutachoka kunyonywa na kudhulumiwa haki zetu hapo ndipo tutapambana nao usiku na mchana ili kukukomboa wewe Tanzania.

No comments: