Jan 4, 2009

Mugabe: Kamwe sitamwamini Mzungu

Asema wazungu kwao si Afrika

Makala
Na Fita Lutonja

“KAMWE sitamwamini Mzungu hata siku moja, mweupe pekee wa kumwamini ni yule aliyekufa, wazungu kwao si Afrika, Afrika ni ya Waafrika hivyo basi Zimbanwe ni ya Wazimbabwe”

Huo ni usemi wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (84) ambao amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akiutumia kila wakati kuonyesha msimamo wake kwamba hababaishwi na mataifa ya Magharibi na hayaamini kama mataifa hayo yana nia nzuri na bara la Afrika.

Rais huyo amekuwa adui wa mataifa hayo kutokana na misimamo yake ya uongozi. Wanachokiona watu wa Magharibi ni kwamba rais Mugabe ni Mbale anayetumia madaraka vibaya kwa kutetea rasilimali za Wazimbabwe ili zisichuliwe na Mataifa hayo ya Magharibi.

Kwa msimamo wa Mugabe ni dhahili kuwa Rais huyo amedhamilia kutetea rasilimali za nchi yake ili zisichukuliwe na Mataifa ya Ughaibuni ambapo pia amenukuliwa akisisitiza kwa kusema kuwa “Ardhi ni yetu na wala si ya Ughaibuni tumeichukua na kuwapa watu wanaostahili”.

Rais huyo alisema hayo wakati alipoamru wazungu wapokonywe ardhi walikuwa wanaimiliki nchini Zimbabwe na wapewe wazawa wa nchi hiyo.

Msimamo wake daima amekuwa akionyesha kwamba si sahihi kwa mtu Mweupe kumiliki ardhi ya bara la Afrika huku wazawa wakihangaika hawana hata sehemu ya kulima.

Anachoamini Mugabe ni kwamba Afrika ni kwa ajili ya Waafrika, msimamo wa aina hiyo umekuwa ukimweka katika migogoro na mataifa ya Ulaya na Marekani.

Hata nchi yake ilipowekewa vikwazo vya kunyimwa misaada na mataifa hayo ya Ulaya na Marekani ambapo ilipelekea Zimbabwe kuwa na hali mbaya kiuchumi, rais Mugabe hakutishika na hilo bali aliendelea kutamba kwa kusisitiza “Kamwe hatutaanguka, acha ukame uje, umasikini nao uje, lakini asilan hatutaanguka daima”

Usemi wa Mugabe unaonyesha kuwa anamsimamo na fikra kubwa za kujua kuwa nchi yake haitajengwa kwa misaada kutoka ughaibuni bali itajengwa na Wazimbabwe wenyewe kwakutumia rasilimali zao.

Pia msimamo huo unaonyesha kuwa haitatokea hata siku moja wazimbabwe wakapiga makoti kwa mataifa ya uhgaibuni ili wapate misaada ambao ya kiunyonyaji kwa sababu misaada hiyo inalenga kuiibia Zimbabwe rasilimali zake. Kwa Mugabe hilo kamwe anasema halitatokea hata situ moja.

Mugabe hataki kuhusudu misaada kutoka ughaibuni wakati akijua kuma Mataifa mingine ya Afrika yanavyohusudu likiwemo Taifa laTanzania.

Nikifkria mpaka ninashindwa kujua huyu Mugabe ujasiri wa kuamua kutetea rasilimali za nchi hiyo ameutoa wapi? Huu ujasiri wa Mugabe huwa ninaufanananisha na ujasiri wa Julius kaisar ambapo na yeye kuna kipindi alidiliki kusema kuwa kamwe hawezi kumuogopa Mzungu mwenye kitambi na nywele ndefu bali anawaheshimu sana wanyonge na wanaodhulumiwa haki yao.


Kwa watu wenye mtazamo tofauti wanaweza wakauchukia msimamo wa Mugabe wa “kutokumwamini Mzungu”. Lakini msimamo huu ni wa kweli kabisa na unamantiki sana kwa Mataifa ya Afrika ambayo yanahusudu Wazungu kwa kuwapa ardhi na kila rasilimali, wakati Wazalendo wa mataifa hayo wakiendelea kuteseka na umasikini hohehahe.

Mataifa mengi ya kiafrika kuwapata viongozi kama Rais Mugabe wenye kuzilinda rasilimali za nchi zao zisiendelee kuchukuliwa na Wazungu ni wachache mno.

Labda Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mfumo wa Azimio la Arusha, yeye ndiye anaweza kuwa mfano wa kuigwa katika kutetea rasilimali za Wazalendo kwa kuazisha mfumo wa utawala wa Azimio la Arusha ambalo lilikuwa na misingi ya kuhakikisha Watanzania wanafanyakazi bila kutegemea misaada kutoka kwa Mataifa mengine, Mwalimu aliwahi kusema “Tanzania daima itajengwa na Watanzania wenyewe na haiwezi kujengwa kwa misaada ya Mataifa mengine”

Mugabe kwa msimamo wake wa kutetea rasilimali za nchi yake zisiibiwe na Wazungu, ni dhahili kuwa kiongozi huyo sasa ametambua kuwa Afrika bado hajajikomboa na kupata uhuru wa kweli bali iko katika ukoloni wa kiunyonyaji ambao ni "Ukoloni Mamboleo"

Ukoloni huu unaimaliza Afrika taratibu bila viongozi wa nchi hizo kutambua kuwa nchi zao zinafirisiwa kiujanja na Mataifa hayo ya Ughaibuni.

Katika bara África Rais Mugabe peke yake ndiye anayeonekana kulinda rasilimali za nchi yake kwa manufaa ya wazalendo wa nchi hiyo, ambapo ni ishara kubwa ya kuonyesha anataka kuikomboa nchi yake kutoka katika ukoloni wa kiunyonyaji uchumi "Ukoloni mamboleo" ambao Mataifa yote ya afrika yanauhusudu na kuupigia magoti ndio maana yanaendelea kunyonywa kila kukicha huku yakiendelea kuwa masikini ya kutupwa.

Lengo kuu la Mugabe ni kutaka kuona Zimbabwe ikiwa huru na inajengwa na rasilimali zake na sio kutegemea misaada mbalimbali kutoka katika Mataifa yalioendelea ambayo lengo kuu la Mataifa hayo ni kutoa misaada ya kiunyonyaji ili wachukue rasilimali za Waafrika.

Hatukatai kuwa uchumi wa Zimbabwe umeyumba, katika kipindi hiki kutokama na mataifa hayo ya ughaibuni kusitisha kutoa misaada mbalimbali katika nchi hiyo, jambo hili la kunyimwa misaada Zimbabwe ni jambo ambalo Wazimbabwe wanatakiwa kuelewa kuwa wanachotakiwa sasa ni kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Zimbabwe wanaitoa katika ndimbi la umasikini ni sio kutegemea misaada ya kiwiziwizi yenye mlengo wa kudidiniza uchumi wao.

Wazimbabwe wanatakiwa waondoe fikra ya kutawaliwa na kuwa tegemezi kama mataifa mengine ya Afrika, kwani sasa hivi wanachotakiwa kutambua kuwa wako huru na rasilimali zao katika kuzitumia tofauti na mataifa mengine ambayo bado yametawaliwa kiuchumi huku yakiendelea kunyonywa.

Jambo la Zimbabwe kujikomboa kutoka katika unyonyaji huu ni jambo la kufurahia kwa sababu uhuru huo ni Zimbabwe peke yake ambayo imeupata kati ya nchi zote za Afrika.

Ninaimani wazimbabwe mabadiliko ya ghafra ya kupata uhuru wenu yamewapa usumbufu mkubwa kutokana na kupandikizwa fikra tegemezi za Wazungu zilizowafanya kusahau kujitegemea mkahusudu misaada wakati rasilimali yenu inaibiwa bila kujitambua.

Kwa hiyo mabadiliko haya mnatakiwa mshangilie kwa kuwa uhuru wa nchi yenu umepatikana na mnatakiwa kuondoa fikra tegemezi mulizopandikizwa na wazungu na kuwapumbaza ili waendelee kuwanyonya rasilimali zenu, huku wenyewe Wazungu wakiendelea kiuchumi katika nchi zao na nyinyi munaendele kuwa na umaskini na fikra tegemezi.

Kumbukeni ya kwamba katika kitabu kitakatifu Bibria inatuambia kwamba wakati Mussa anawakomboa wana wa Israel kutoka katika utumwa wa nchi ya Misri, walilalamika huku wakimraumu Mussa wakisema, “Mussa amewatoa katika nchi ya neema nyenye asali na maziwa amewapeleka nchi ya Kanan ambayo ina njaa na mateso ya kila aina”.

Hawa wana wa Israel walikuwa wamezoea kunyonya na kutumikiswa na Wamisri kwahiyo mabadiliiko ya kutolewa Misri yaliwapa shida Wana wa Israel.

Lakini walipozoea waliona kuwa kumbe kweli walikuwa ndani ya utumwa bila wao kujua.

Na nyinyi Wazimbabwe yawapaswa musiendelee kulaumu na kulalamika ya kwamba Mugabe kawafukuza Wazungu kutoka katika nchi yenu kuwa amefanya makosa. La hasha! hajafanya makosa mbali ameamua kuwakomboa kutoka katika utumwa wa kizungu.

Msihudhunike na kufadhaika mioyoni mwenu ya kwamba Zimbabwe imekoswa misaada. Hiyo misaada ilikuwa ya kiunyonyaji kwa sababu ilikuwa inatumika kama ngao ya kuwatuliza msije kugundua wizi wa mchana wa Wazungu ambao wanaufanya katika Mataifa ya Afrika.

Kumbukeni ya kuwa uchumi wa Zimbabwe hauwezi kujengwa na Mataifa kutoka Ughaibuni hata siku moja haitatoke kamwe! Hivi ebu jiulizeni tangia lini nchi nyingine akajenga uchumi wa nchi nyingine?

Wazimbabwe wanachotakiwa ni kufanya kazi kwa kutumia rasilimali zao katika kuhakikisha wanaondokana na umasikini kwani bahati kubwa waliyoipata ya kujikomboa kutoka kwa wezi wa mchana wazungu ni bahati kubwa mno.

Afrika imefanywa kama kitega uchumi cha kuendeleza nchi za ughaibuni! Afrika imefanywa ndio sehemu ya kuchukua utajili na kuuhamishia katika Mataifa ya Ughaibuni! Afrika imefanywa kama mtaji wa kuendeleza uchumi wa nchi za Ughaibuni! rasilimali za afrika kama vile dhahabu, almas, ulanga, Tanzanite nk. zimekuwa mtaji wa kuendeleza na kukuza uchumi wa Wazungu. Kwa mtindo huu lini tutajikomboa kiuchumi?

Mbona hawa wazungu wanaione sana Afrika? Tangia enzi za zamani wanaidhulumu bila hata kutuhurumia! Walitufanya watumwa wakatuuza kwa mataifa ya mbali. Hawakulidhika na hilo wakaamua kututawala bila ruhusa huku wakaendelea kutunyonya.

Na baada ya kuondoka katika harakati za kudai uhuru wa bendera waliondoka huku wakiwa na kinyongo ndio maana tena wamekuja na njia nyingine ya kutunyonya ya ukoloni mamboleo.

Tukikataa huu ukoloni mamboleo wanatutishia kutunyima msaada? Hawa watu katu si wa kuwaamini hata siku moja!
Mwisho.
Nipigie: +255 764 992264
Niandikie: fitazi@hotmail.com
Nitembee: http://www.fitalutonja.blogspot.com/