Aug 29, 2008

Saa ya ukombozi

Wakati umefika wa kujiuliza, kujitafiti, kujinasua na kujikomboa kutoka kwa hawa wanyonyaji makupe wanaotumia jasho letu kutunyonya ili wao waendelee kuwa matajiri, yatupasa kujiuliza kwa kina na fikra za kimaendeleo sasa tufanyeje? Kwani wa kutukomboa sasa hayupo tena kwani Azimio la Arusha mtetezi wa haki halipo tena!!! Wale makupe ngunguni wamelihujumu ili watunyonye kweli na sisi tunakubari Azimio la baba wetu Hayati Mwalimu JK Nyerere liondoke kwa sababu Mwalimu hayupo?

Tusikubari yatupasa kushika kila kitu kurudisha Mkombozi wetu Kipenzi Azimio la Arusha kwani alikuwa analinda maslahi yetuna jasho letu lisitumiwe na Wanyonyaji wa nguvu za umma, yatupasa kujiuliza ni lini tutajikomboa na kutoka katika Utumwa wa hawa Mabeberu wanyonyaji?

Sisi wenyewe ndio tunaweza kujikomboa kwa Azimio lilitufundisha Ujamaa na Kujitegemea kwahiyo tusisubili watu wengine watukomboe hayupo wa kutuhurumia tupambane ili tulirudisha Azimio la Arusha liunguze tena vikaragosi na kuleta ujamaa wa kweli. Ndugu wanaharakati, mashika ya dini, mashikaka mengine malimbali, na watanzania wote tupiganieni azimio la baba wa Taifa tuhakikishe tunalirudisha na kanuni zake za kukata milija kwa Mabwanyenye.

Tusiposimama imara kwa hili wataendelea kumdhalilisha baba wetu wa Taifa kwa kuvunja haki za utawala bora wenye kujali kila masilahi ya umma