Aug 22, 2008

Tanzania Wanakutolea macho

Tanzania mbona wanakutamani kila sehemu ya dunia? Mabeberu na Mabepari wametoa macho juu yako, huku wakija kwa nguvu wakitaka kukudhulumu haki yako wengine wanajifanya kuwa rafiki zako ili wakudhulumu raslimali zako ulizonazo, wanakudanganya kwa kukupa zawadi ndogo ili kukupumbaza, wakuibie.

Ninajiuliza ni kitu gani ulichonacho mpaka wanakutamani na kutaka kukuibia? Aaah kumbe ni raslimali zako ndizo wanazitamani!! basi unasitahili pole na kuhurumiwa sana Tanzania.

Angalia sasa ulipowakubali na kuwapokea kwa mikono miwili wameanza kukudhulumu mali yako na kupeleka ughaibuni huku wakikuacha wewe umejikaukia ka!! bila hata huruma. Kukauka kwako kumekufanya uwaombe misada hao wezi wa mali yako, napo unapowaambia wanaaza kukucheka na kukusema Ehee!! Eti wewe ni maskini omba omba wakati wao ndio wamekukausha na kukufirisi raslimali zako, lakini usijali Tanzania wangu nikupendae kwani hohehahe hakoswi siku yake, ipo siku tutachoka kunyonywa na kudhulumiwa haki zetu hapo ndipo tutapambana nao usiku na mchana ili kukukomboa wewe Tanzania.

Tanzania ya dhamani

Tanzania wewe ni wa dhamani sana hakika Mwenyezi Mungu alikujaria na kukubaliki tena kwa upendeleo, kwani kila kitu alikupatia, madini ya kila aina alikupa, mito na maziwa ya maji na zenyewe alikubariki, mbuga za wanyama kubwa zenye kuvutia kila aina ya watarii, ardhi yenye rutuba sanjari na milima mbalimbali ukiwemo mlima mrefu kupita yote Africa Kilimanjaro alikupa hakika wewe Tanzania umebarikiwa.

Lakini mimi ninakushangaa Tanzania pamoja na vitu vyote hivyo bado unaendelea kuisha na kubakia mashimo kila sehemu, huku madini wakikunyang`anya na kupeleka ughaibuni kama wewe huna watu wako!!?? hakika ninakusikitikia Tanzania wangu kwa jinsi unavyokaukia na kukonda huku ukibaki mifupa tupu!!!! samaki wako sangara wanakwapuliwa, pesa za walipa kodi wako zinafisadiwa na mafisadi wahujumu mali zako, ooooo!!!!! Ona sasa umebaki maskini huku ukiwayawaya huna pa kukimbilia!!

Ninazidi kushangaa sana wale waliokunyonya wanatembelea benzi, crusser,prado vx zenye mabillioni ya pesa zako ukiwasachi kwenye mabegi yao wanayotembea nayo yamejaa pesa zako huku wakiendelea tena kukutwisha mzigo kichwani wa makapuni yanayokufirisi, huku wewe ikibaki umekonda huna hata kitu cha kuwapa Watanzania!! Sasa yakupasa upambane na wanaokufirisi kwani watu wako watakufa kwa njaa. Haya jamani Watanzania simameni kuikomboa Tanzania Dr. Wilbroad Slaa simama, Zitto Kabwe inuka, Anne Kalango, Harisoni Mwakyembe, na wanaharati wenzanu simameni kupambana, Tanzania inaisha huku tunaiona mafisikoko wanaitafuna bila huruma kabisa.