Sep 24, 2008

Ipo siku haki yetu itapatikana.


Aliyevunja Azimio la Arusha ana hatia kubwa

Makala

Fita Lutonja

NINAIKUMBUKA Februari 5, 1967 kama ni siku ya ukombozi wa wanyonge na changamoto ya kuongeza fikra za maendeleo miongoni mwa Watanzania, kwani siku hiyo kule Arusha, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alitangaza kukomesha watu waliozoea kunyonya jasho la wanyonge bila huruma.

Hakika siku hiyo ilikuwa ya neema kwa Watanzania, kwani mfumo mpya wa utawala chini ya Azimio la Arusha, uliashiria nyota ya matumaini ya kujikomboa kwa wanyonge na waliokuwa wanadhulumiwa haki zao.

Baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961 na kuwa Jamhuri mnamo mwaka 1962, na hatimaye kuungana na Zanzibar mnamo mwaka 1964 na kuunda Tanzania, hatukuwa na maendeleo makubwa.

Lakini Mwalimu kwa kuona baadhi ya viongozi kuwa bado wana fikra za kinyonyaji kama walizokuwa nazo wakoloni, akaamua kuanzisha Azimio la Arusha lililokuwa na misingi ya kulinda haki za wanyonge na kuondoa dhuluma ya tabaka la wanyonyaji.

Mwalimu aliona kipindi hicho umma wa Watanzania ukidhoofishwa kwa kudhulumiwa haki na tabaka la mabeberu na mabwanyenye ambao wengi wao walikuwa ni viongozi serikalini, kitendo hicho cha viongozi kuwanyonya wanyonge kilimkera sana.

Dhuluma haikuwa siri kipindi hicho, viongozi waliwadhulumu Watanzania waziwazi bila hata aibu, huku wakijiona wao ni bora zaidi ya wanyonge, wakiendelea kujikusanyia mirija mirefu ya kunyonya mali na haki za watu wengine. Waliendelea kuwakashifu walipa kodi kwa kuwanyonya jasho lao bila hata kuwahurumia.

Haikumchukua muda Nyerere kubaini kuwa ndani ya serikali yake changa, kuna wanyonyaji; mabepari na mabwanyenye ambao hawakuwahurumia wananchi wanyonge wa kawaida.

Alitambua kumbe ubepari na unyonyaji si rangi ya mtu tu. Ilionekana wazi kuwa hata watu weusi wanaweza kuwa wabaya kama walivyo Wazungu.

Baada ya kuona kuwa wanyonge wanadhulumiwa haki zao, tena hadharani, Nyerere aliamua kulinda haki yao ili isiendelee kudhulumiwa.

Aliunda Azimio la Arusha kama misingi ya kuhakikisha kuwa haki ya mnyonge inalindwa kama inavyolindwa haki ya mwenye nguvu. Aliliwekea Azimio kanuni za kuhakikisha hilo linatendeka.

Ni kweli kuwa Azimio lilisaidia kuleta usawa katika jamii. Kupitia Siasa ya Ujamaa, Azimio la Arusha lilifanikisha wanyonge nao kujiona kuwa wana fursa ya kufaidi matunda ya uhuru. Ujamaa na Azimio liliwataka viongozi kuwa wajamaa kweli, wakiwaona watu wanaowaongoza kama ndugu.

Hii ilisaidia kujenga utawala bora, unaoheshimu misingi ya utu badala ya unyonyaji. Hakukuwa na mtu dhalili na mtu bora. Unyonyaji ulionyeshwa kuwa ni mbaya.

Azimio la Arusha pamoja na misingi yake kwa watumishi wa umma, vilevile lilisisitiza ujamaa kuwa ni imani na njia pekee ya kuondokana na ubaguzi, ubinafsi na dhuluma, na kuwafaidisha wananchi wa aina zote nchini. Azimio, pamoja na Ujamaa viliamsha mori na ari ya kufanya kazi kiasi kwamba nchi ilifanikiwa kujijenga kwa kiasi kikubwa.

Watu walifanya kazi kwa kujitolea na kuanzisha vijiji vya ujamaa hadi viwanda. Tanzania ikageuka kuwa mzalishaji wa bidhaa zilizohitajika sana kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo.

Azimio lilikuwa na siasa ya kujitegemea pia, ambayo iliboresha utumishi wa umma na uajibikaji wa viongozi na wananchi wa kawaida. Siasa hiyo ilimtaka kila mtu katika nafasi yake, kuhakikisha anazalisha kwa wingi, ili kuepuka kutegemea mtu mwingine.

Hii ilianzia kwa mtu mmoja mmoja mpaka kwa taifa. Taifa nalo lilitakiwa kujitegemea kwa mahitaji yake yote muhimu.

Watu walitakiwa kuwa na fikra kuwa wanaweza kuendesha maisha yao binafsi, au nchi bila hata kutegemea nchi nyingine. Tofauti na sasa, ambapo Azimio limeuawa, nchi imekuwa ni kama ombaomba. Jinsi ambavyo wanavyoongezeka ombaomba wa mitaani, na nchi nayo inazidi kuwa ombaomba na inakuwa kama inashindana na ombaomba wa mitaani.

Sasa hali imebadilika baada ya Azimio la Arusha kuuawa na kuzikwa. Hali imezidi kuwa mbaya na kwa hakika, aliyeliua Azimio la Arusha anastahili kubebeshwa lawama zote na hata ikibidi alaaniwe.

Mtu huyo anapaswa kubeba lawama zote kwa sababu amewasababishia mamilioni ya Watanzania maisha magumu.

Hivi sasa Watanzania wameshaanza kushuhudia unyonyaji na unyanyasaji ndani ya nchi yao wenyewe, licha ya kuwa walipata uhuru miaka zaidi ya 40 iliyopita.

Unyonyaji umerudi kwa kasi kwa njia ya uwekezaji.

Wawekezaji wamegeuka kuwa wanyonyaji ambao wanakamua mali za Watanzania bila huruma.

Watanzania, ambao nchi yao ina rasilimali zisizohesabika, leo wamekuwa wanyonge kama watu wanaoishi jangwani kusiko na kitu chochote.

Hadi hii leo sijaelewa nini ilikuwa misingi ya kuvunja Azimio la Arusha. Na misingi hiyo ilikuwa na masilahi gani kwa umma wa Watanzania?

Inashangaza kuwa wakati Azimio la Arusha lilipoundwa, wananchi walielimishwa maana na faida zake. Lakini walipoamua kulivunja, hawakutokea hadharani kueleza sababu za kufanya hivyo!

Mwalimu alifanya mikutano na kuchapisha vitabu na makala mbalimbali, yote akilenga kuwaelimisha wananchi wa kawaida kuhusiana na mfumo huu mpya wa maisha yao.

Lakini wenzetu hawakuona umuhimu wa kuwaeleza wananchi kwa nini waachane na mfumo wa maisha ambao wamekuwa wakiishi kwa miongo minne iliyopita.

Kimyakimya walikusanyika Zanzibar na kufanya maamuzi makubwa huku Watanzania wenyewe wakiachwa gizani. Kwa nini wananchi hatukuulizwa kabla ya kufikia uamuzi wa kuvunjwa kwa Azimio la Arusha? Au kwa nini mlipoamua kulivunja hamkurudi tena kwetu kutueleza ni kwa nini mmefikia uamuzi huo?

Au mlipoingia madarakani mliona hamupati nafasi ya kutuibia na kutunyonya haki yetu kwa sababu ya kanuni za Azimio la Arusha ziliwabana?

Kwani Azimio la Arusha lilikuwa na kasoro gani? Hivi kutetea haki za wanyonge nacho ni kitu kibaya? Mbona hamkutueleza hizo kasoro?

Azimio la Arusha, lililokataza viongozi kumiliki mali kupindukia limevunjwa na matokeo yake tumekuwa na viongozi mafisadi.

Au sijui ni mafisadi viongozi, maana ni vigumu kujua, kwa sababu wapo viongozi ambao walianza ufisadi kabla ya kupata uongozi na wakatumia mali zao kusaka uongozi, pia wapo viongzoi ambao walitumia nafasi zao kujilimbikizia mali na kuwa mafisadi.

Watu sasa wananyonywa na viongozi wao, dhambi ile ile ambayo Nyerere aliiona na kuiwekea kanuni za kuikataa.

Leo inakumbatiwa na wananchi wamekosa mtetezi kwa sababu viongozi ambao walipaswa kuwa watetezi wao, ndio wanaoongoza kundi linalowanyonya.

Azimio lenu la Zanzibar limeleta nini kwetu sisi Watanzania wa hali ya chini? Mbona limezidi kutuumiza na kutuletea maisha magumu na kutufanya tuwe wanyonge zaidi?

Sasa hivi masuala ya dhuluma, unyonyaji, umwinyi sanjari na ufisadi ndani ya serikali ni vitu vya kawaida.

Walidhani kuwa umaskini uliokuwepo ulikuwa unaletwa na Azimio la Arusha, wakaliua ili kutokomeza umasikini.

Lakini hali ya mambo imethibitisha kuwa hilo si kweli kwa sababu umaskini badala ya kutoweka, unaongezeka.

Na inavyoonekana ni vigumu sana kukuza uchumi wa nchi kwa mfumo walioukubali. Sana sana wanachofanya ni kujenga uchumi wa watu binafsi.

Tunatawaliwa kwa mfumo mpya wa ukoloni mamboleo. Tofauti yake na ukoloni tulioung’oa mwaka 1961 ni ndogo sana lakini madhara yake ni makubwa kuliko ya ule tulioukataa zamani.

Uhuru wetu sasa umegeuka kuwa wa bendera, jambo ambalo Azimio la Arusha lilikuwa linapiga vita kupitia kanuni zake.

Mwalimu katika mkutano wake wa kuelezea ubora wa Azimio la Arusha aliwaambia Watanzania ya kwamba jambo muhimu ni kujitegemea.

Aliwaambia Watanzania kuwa hawapaswi kumtegemea mtu mwingine yeyote. Tumeliua Azimio la Arusha na tumeingia katika mtego wa kuwategemea wafadhili na wahisani!

Azimio lenu la Zanzibar, ambalo kimsingi linatetea viongozi, limetuletea aibu ndani ya nchi yetu kwa viongozi wa umma kujimilikisha mali ya umma kwa kisingizio kuwa ni ujasiriamali.

Azimio lenu la Zanzibar tunalilaani kwa sababu limetuletea EPA, Richmond, unyonyaji, ubeberu, dhuluma, ufisadi, na matatizo chungu nzima ambayo yote haya tungekuwa na Azimio la Arusha yasingetokea kwani misingi yake ilikuwa hairuhusu.

Viongozi wanapswa kutambua kuwa wananchi wamechoka kweli na EPA, Richmond , unyonyaji, ubeberu, ubepari, ukupe, ukiritimba, umwinyi na wanachotaka ni Azimio la Arusha la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na misingi yake ya utawala bora, ili liunguze tena viongozi vikaragosi waliozoea dhuluma.

Idumu nguvu ya haki:
nipigie:0764 992264

Sep 20, 2008

Toa Maoni kwani ni uhuru wako


Huyu ni Sophia Kessy mtangazaji mahiri na mwenye sauti yenye kuvutia kwa kila msikilizaji. kwani katika kipindi chake cha Afikani mbambata ndani ya nyumba ya clouds Fm huwa anatisha, mwanadada kweli amejaliwa kipaji chake.

Sep 18, 2008

Toa Maoni

Hapa ni mimi siku hiyo nachukua picha hii nilikuwa na rafiki yangu Dora Sanga ambaye ni mfanyakazi mwenzanzu.

Haya:




Huyo naye anaitwa mic is just my friend naye and nampenda pia na yeye ananipenda japo kuwa hana ufikra wa kunishauri sana maana anapenda tuongelee masuala yasiyo na faida lakini mimi nimeshazoe kuongelea mabo muhimu kama wazungu wanavyodai kuwa non skilled people always talk about themselve, little skilled people talk about other peole and skilled and serius people talk about development and how to solve problem for progress achieve

Sep 15, 2008

Toa Maoni

Huyu ni rafiki yangu anaitwa Gloria anakaa Marekani ni mojawapo wa marafiki zangu niwapendao sana katika maisha yangu ila huyu ninampenda zaidi kwa sababu ana huruma kwa kila mtu, na sasa hivi ananitafutia visa ya kwenda Marekani kufanya kazi huko kulingana na kuniambia kwa muda mrefu nimeamua kumkubalia ombi lake kwenda kwa hiyo hivi karibuni akikamilisha kuwasilianasa na ubalozi wetu atanitumia hiyo visa ili niruke, ila sitaisahau Tanzania na mafisasadi wake nitahakikisha nikisitafu kazi yangu huku nije Tanzania kupambana na mafisadi ili kurudisha heshima ya wanyonge haya: BlockquoteMungu nibariki mimi mubariki rafiki yangu Gloria na mwisho Mungu ibariki Tanzania.

Sep 13, 2008

Toa Maoni yako





Anaitwa Markus Mpangala mwanafunzi chuo kikuu cha Dar rafiki yangu mkubwa sana na sijapata rafiki mwenye mawazo na fikra za maendeleo kama yeye hakika amenishauri mambo mengi sana katika maisha yangu na wmengi aliyonishauri leo hii yameniletea maendeleo katika maisha yangu.
Kwa sasa hivi mimi na yeye wote ni wandishi wa habari katika magazeti mbalimbali hapa nchini vilevile wote ni Wanablogu tunaohakikisha kila mtu dunia nzima anapata habari kupitia blogu zetu

Toa Maoni yako




Huyu ni rafiki yangu Habiba anakaa Dar ni rafiki yangu wa karibu sana kwani huwa ananishauri pale ninapokwanma kimawazo na kifikra hakika sitamusahau na wewe kama unamatatizo niombe contact zake ili upate ushauri daima huwa hatozi kitu chochote ni mjamaa wa kweli nas na fikra za kiujamaa. Basi ndugu toa maoni kuhusiana na ulivyomuona na maelezo yangu

Toa Maoni yako.


Huyu ni mwanaglogu mwenzangu je, unamonaje? toa maoni yako kuhusiana na unavyomuona hapo kwenye picha ila mimi huwa ninajifunza mambo mengi kutoka kwake. Muangalie hivyo tuni mwanadada nzuri kwanza anavutia na anaakili nyingi sana na ni mtu wa malengo na maisha yake.

Sep 11, 2008

Ukombozi wa haki ni uhuru wa habari

MAKALA

KWA misaada mbalimbali ya habari tunaona historia ya mawasiliano ya umma ilianza mwanzoni mwa utamaduni wa watu walipokuwa wanawasiliana na mfumo wa ishara baadaye wakawa wanawasilia kwa mdomo kipindi hicho kulikuwa hakuna lugha ya kuandika , kwahiyo mawasilia yalifanyika pale watu wanapoonana oso kwa uso

Kipindi hicho watu walikuwa wanaishi kwa kutegemeana lakini kulingana na muingiliano wa jamii mawasiliano yalihitajika sana mwingoni mwa jamiiambapo mawasiliano hayo kulingana watu kuhitaji kuwasiliana, mawasilano hayo hayo yalihitaji teknolojia zaidi ili kukidhi mahitaji ya jamii.

Miongoni mwa miaka ya 5,000 kabula ya Christo sehemu mbalimbali binadamu waligundua herufi mbalimbali kama kule Misri watu wa kule waligundua herufi za kutumia picha ambazo walikuwa wanatumia katika kufikishana ujumbe. Huko China watu wa kule waligundua herufi mbalimbali ambazo walitumia katika mawasiliano yao, hii yote inatudhihilishia kuwa watu walihitaji sana kuwasiliana na inatuonyesha kuwa mawasiliano ni ya muhimu katika jamii hayapaswi kupuuzwa hata kidogo kama yanavyopuuzwa Tanzania.

Halikadhalika siku zilivyozidi kwenda ndio watu walivyokuwa wanahitaji zaidi mawasiliano miongonui mwao hapo ikaja pale Mwanamapinduzi Mhunzi wa vyuma Johannes Guernberg alipokundua mashine ya kuchapisha herufi ambayo ilisaidia sana watu katika kuwasilia kwa kuandika hizi ni changamoto zilizojitokeza ili kuhakikisha binadamu anapata mawasiliano.

Ugunduzi wa Guternberg ilivuta hisia kubwa sana miongoni mwa jamii ambapo watu wengi walikubali ugunduzi wake. Mitandao mbalimbali inatuambia miongoni mwa watu waliokubali kazi ya Guternberg ni Mwanaharakati Marshall McLuhan ambaye alielezea kuhusiana na kazi ya Guternberg katika kitabu alichokiandika mnamo 1962 huku akikiita kw jina la “The Guternberg Galaxy” katika kitabu hiki McLuhan alielezea kiundani zaidi umuhimu wa ugunduzi wa Guternberg katika mfumo mzima wa mawasiliano.

Mitandao inaendelea kutuhabarisha kuwa uvumbuzi wa Guterberg ulipelekea kujitokeza kwa uandishi wa habari ambapo ilipelekea kuanzishwa kwa machapishi mbalimbali, kuko Kaisari Roma kulianzishwa gazeti la Acta Diurna na sehemu mbalimbail kama huko Holland mwaka 1920 kulianzishwa gazeti la Corantos. Hii yote ilikuwa ni kupanuka kwa mawasiliano kutokana na mahitaji ya binadamu, ambapo ilipelekea baada ya muda kujitokeza kwa uandishi wa habari na vyuo mbalimbali za uandishi wa habali zikaanzishwa, ilikuweka mbele umuhimu wa mawasiliano na kuwawezeshha waandishi kuwa makini na kazi yao.

Kulingana na kupanuka kwa mawasilano ya habari kwa kutumia vyombo vya habari na vyuo vya uandishi wa habari kuongezeka Taaluma hii ya habari ilipata umuhimu zaidi na kuleta changamoto kubwa sana miongoni mwa jamii. Huko marekani taaluma ya habari ilitiliwa maanani sana, siyo tu Marekani hata nchi zingine ziliona umuhimu wa taaluma hii yenye kutumia hakili na busara, kuwa ni miongoni mwa taaluma ya muhimu sana katika jamii. Baada ya kuelezea hayo hapo juu kama nilivyokufahamisha hapo mwazo kwamba nimetumia vyanzo vya habari mbalimbali ikiwemo mitandao.

Ninakuja sasa Tanzania. Je, hii taaluma tunaidhamini kama nchi zingine? Tunaipa heshima kama taaluma zingine kama vile udaktari, ualimu, uchumi, uongozi, Uanasiasa, utaalamu wa miamba, uiginia, nk? Tanzania hii taaluma ya habari haidhaminiwi, inatukanwa, inadharauliwa, inanyongwa hadharani, kudharauliwa hivyo ndio inapelekea taaluma hii kuonekana dampo kwa kila Mtanzania, ninaposema dampo musinielewe vibaya mbali ninamaana ya kuvamiwa na kila mtu na kujiita Mwandishi wa habari. Ninarudia tena kusema kuwa taaluma hii Tanzania ni dampo, kweli hii taaluma ni dampo kabisa, tena lile dampo lenye kila aina ya takataka mbalimbali zikiwemo zile zinazonuka vibaya sana.

Hii inashangaza sana kwa nchi kama Tanzania kutothamini taauma ya habari ambayo ni taaluma muhimu sana ndani ya jamii kwani taaluma hii ndio mfanisi mkuu wa kuhabarisha Taifa katika nyanja mbalimbali kama vile za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kisaikulojia, kijeshi nk. Inashangaza sana kwa taaluma hii nyeti hapa Tanzania kuingiliwa na kila mtu kuanzia mtu wa darasa la saba utakuta ni Mwandishi wa habari na tena kaajiliwa na chombo cha habari. Huyu mtu darasa la saba hana taaluma ya habari atawezaje kuandika habari zenye kuelimisha jamii kama siyo kuidhalilisha taaluma ya habari na kuliweka Taifa katika hari ngumu? Huyu mtu darasa la saba hana upeo na suala zima la habari atawezaje hata kumuuliza maswali Waziri au Mkurugenzi yoyote ili apate habari yenye kuelimisha jamii? Ataanzia wapi kuuliza maswali wakati hajui namna ya kuuliza maswali yenye kupelekea kuandika habari yakinifu yenye faida kwa wananchi na Taifa kwa ujumla? Tunapofanya hivi siku za mbele Taifa litakuwa katika hari gani? Je litaelimishwa au litahatarishwa?

Tanzania kuna mambo ya ajabu kabisa utakuta hata mtu amesoma taaluma nyingine lakini mtu huyo akikoswa kazi katika fani yake anakimbilia uandishi wa habari, huyu atafanyaje kazi ya uandishi wa habari wakati fani yake ni Ualimu au Uasikari kama siyo kupeleka Taifa shimoni na kudidimiza uhuru wa wananchi katika kupata habari za kuelimisha ambazo ni haki yao ya msingi? Wanapokosea hawa watu ambao hawana taaluma hii ya habari si Taifa na Watanzania wote wanadanganywa? Tanzani tusifanye mchezo kwa mambao muhimu katika Taifa kama haya. Kwa nchi kama tanzania si ajabu kukuta chombo kama redio hakina Mwanataaluma wa fani hiyo hata mmoja, hivi vyombo vipo tena vingi!!!!! na vimesajiliwa na serikali yetu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Serikali inasajiri vipi hivi vyombo vya habari bila hata mwandishi na mtangazaji wa habari hizo kama siyo ufisadi ndani ya serikali na vyombo vya habari kwa ujumla? Hii si kufanya taaluma hii kama dampo la kukimbilia watu wa aina mbalimbali na matokeo yake kupata habari za uongo zenye madhara katika jamii. Serikali ninawaomba muangalie vizuri taaluma hii ya habari kwani musipoangalia mutajikuta munawaandihi wegine kutoka Milembe Dodoma!!!!! Maana uandishi wa habari umezidi kuvaniwa na kila mtu.

Tanzania hii taaluma imekuwa kimbilio la kila mtu (dampo) kwani hata mtu alikuwa anagombania ukisura (usura) akishinda huo usura basi anakuwa mwandishi wa habari na anaajiliwa na chombo cha habari. Hivi kushinda huo usura ndio kamaliza chuo cha uandishi na utangazaji wa habari? Mbona watu hawa wanadhalilisha taaluma ya habari? mbona hawakibilii uhakimu, ualimu au upolisi? Taaluma hii ya habari tunaididimiza wenyewe kwa kutoipa chamgamoto za kutosha na kuidhamini kama taaluma zingime, hii ndio inapelekea kudharauliwa kwa Waandishi wa habari wetu na kudharauliwa huko kunawalenga wanahabari wote kumbe wachafuzi wa taaluma ni wengine ambao hawajasomea taaluma ya habari na hawafuati maadili ya uandishi wa habari.

Kulingana na taaluma hii kuonekana ni taaluma ambayo inavamiwa na kila mtu serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari nchini waweke mikakati ya kudhibiti kuwa na waandishi wasio na taaluma ya habari katika vyombo mbalimbali vya habari hapo ndio tutalinda heshima ya kazi ya uandishi wa habari na wananchi tutawapa haki yao ya kupata habari zinazotakiwa lakini sasa Wananchi tunawnyima haki yao ya kupata habari zenye kuelimisha zilizoandikwa na kutangazwa na waandishi wenye ujuzi na taaluma yao. Tukifanya hivi hakika laana tutazimaliza zak kila siku kutukanwa kwa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya habari, utamatuni na michezo mwaka 2008/2009 iliyowasirisha bugeni inaonyesha dhahiri katika vyombo vya habari kuwa watatekeleza mambo mengi sana likiwemo la kulinda maadili ya uandshi wahabari hili linatakiwa liende sanjari na kuondoa waandishi wachafuzi wa maadili ya uandishi wa habari ili kuwatendea haki yao wananchi ya kupata habari zenye kukidhi mahitaji yao. Musituambie kuwa kazi ya uandishi wa habari inaweza kufanywa na kila mtu, hilo hatukubaliani nanyi hata siku moja, anayesema hivyo daima tutamuona haitakii mema Tanzania au hajui undani wa kazi hii, ama hajasoma uandishi wa habari ndiyo maana inataka kuingiza nchi katika janga ambalo watoto wetu watakuja kulijutia na kulaani kwa nini tulifanya hivyo? daima hii laana tutatembea nayo.

Pamoja na bajeti hii kuwa nzuri ili waandishi wa Tanzania waweze kuheshimika miongoni mwa jamii, serikali kwa kupitia wizara husika inatakiwa kuweka mipaka katika vyombo vya habari kuajili watu wenye taaluma ya habari na kuondoa fikra za kuamini kuwa kazi ya uandishi inaweza kufanya na kila mtu kwani tunapoamini hivyo tunakuwa hatuwatendei haki yao wananchi ambayo wanatakiwa kuipata kupitia vyombo vya habari.. Serikali iwajari wananchi wake kwa kuweka mikakati ya kuwapatia habari zenye mantiki ya kuelimisha, kuwafahamisha, kuwajenga kwa kuweka mikakati dhabiti kwa kuajiri watu wenye taaluma ya habari, kwani hao watu watakuwa wanaujuzi na kazi yao, wanajiamini na kuheshimu taaluma yao, hapa ndipo wananchi watapata habari zenye kuaminika na hii itapelekea kujenga heshima kwa waandishi wa habari .

Bila hivyo waandishi wa habari wataendelea kutukanwa, kunyimwa haki yao, kulaaniwa, kuwekwa kitanzini, kufukuzwa ofisini, kunyimwa uhuru, kudhalilishwa, pamija na kuitwa majina mengi ya kejeli na dhihaka kama vile makanjanja, wachovu, watu wa mishiko, waandishi njaa, chakupewa na mengine mengi wanayoitwa sasa hivi. Kejeli hizi zinawanyima haki yao waandishi wenye taaluma ya habari vilevile zinavunja misingi ya utawala bora Tanzania.

Toa maoni yako kwa kubonyeza sehemu ya maoni chini au nipigie 0764 992264