Oct 8, 2008

Zidumu fikra za Mwalimu

Mwalimu atakumbukwa daima na watu wenye upendo na nchi yao mambo aliyafanya kwa Taifa letu ni fahari ya watanzania. Huwa napata hasira kubwa mno ninapoona viongozi wetu wakizidi kuvuruga utawala bora wa haki kwa kushindwa kumuenzi kwa utawala wake bora wa Azimio la Arusha lililokuwa na misingi ya haki huku likiwa linakataa dhuluma ya viongozi likitulinganisha viongozi na watu wengine ni sawa.

Natamani siku moja nirudishe heshima ya Mwalimu na ninandoto za kurudisha hii heshima ya Mwalimu kwa watanzani ili watanzania wenzangu waishi kwa amanipasina kunyonywa na Mabeberu yalituzunguka, na ninuhakika ipo sikunitairudisha heshima ya Mwalimu, ninaumia mno ninapoona viongozi wakivunja yale aliyoyakataa Mwalimu BlockquoteDaima zidumu fikra za Mwalimu

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Maneno mazuri sana na pia ndoto nzuri kwani haupo peke yako tupo pamoja. Nami nasema zidumu zaidi na zaidi fikra za mwl. Ndiyo kwa kweli roho zinauma sana kuona viongozi hawafanyi kila wanachotakiwa kufanya.