Fikra za Mwalimu baba wa Taifa zidumu, hakika Mwalimualikuwa na fikra za kimaendeleo, alikuwa mtu wa watu, alikuwa kiongozi anayestahili kuigwa na jamii ya viongo, sasa tunaelekea katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo chake huyu baba wetu wa Taifa nawaomba wananchi wenzangu tujitokeze kumuenzi Mwalimu.
Na walaaniwe wale wote waliovunja uongozi bora wa Mwalimu kwa kulizika Azimio la Arusha na misingi yake yote ya utawala bora, Watanzania tuungane wote kwa pamoja kumlaani huyoaliyevunja Azimio la baba kwani umaskini wetu wote huu ni chanzo chake yeye aliyevunja Azimio, lakini shida tunazozipata watanzania kwa ajiliya kuvunja utawala bora wa Azimio la Arusha ule wake kwa kutuletea hizi shida daima Mungu atamuhukumu kulingana na kutusababishia utawalawa dhuluma.
2 comments:
Ni kweli kabisa watanzania wote tushikamane/ tuuungane. Tusisahau fikra za Mwalimu
Kweli jamani watanzania tufuate fikra za mwal. na ni kweli uhuru ni haki.
Post a Comment